Breaking


Jumatano, 4 Februari 2026

RAIS SAMIA AUNGANA NA VIONGOZI WA DUNIA DUBAI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki mjadala wa ngazi ya juu katika Jukwaa la Serikali za Dunia (World Governments Summit – WGS 2026), lililofanyika tarehe 4 Februari 2026 katika kituo cha Madinat Jumeirah, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).


Ushiriki wa Rais Samia katika jukwaa hilo muhimu umeendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya majadiliano ya kimataifa, hususan katika masuala ya uongozi, maendeleo endelevu, ubunifu wa kiutawala na ushirikiano wa kimataifa. Jukwaa la WGS hukutanisha viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wataalamu kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo.


Kupitia ushiriki wake, Rais Samia ameendelea kuonesha dhamira ya Tanzania katika kujenga uchumi imara, diplomasia ya kiuchumi na nafasi ya nchi katika mwelekeo wa maendeleo ya dunia ya kisasa.


Hakuna maoni: