Breaking


Alhamisi, 5 Februari 2026

VIDEO: MFUMO WA TAIFA WA ANWANI ZA MAKAZI: NGUZO MPYA YA UCHUMI WA KIDIJITALI NA BIASHARA MTANDAONI TANZANIA

Mfumo wa Taifa wa Anwani za Makazi unaendelea kujidhihirisha kama nguzo muhimu ya uchumi wa kisasa, ukiwa chachu ya kukuza biashara, kuboresha utoaji wa huduma za umma na kuimarisha ujumuishaji wa kifedha nchini. Kupitia mfumo huu, biashara nyingi zinaingia rasmi kwenye mfumo wa kisheria huku shughuli za kiuchumi zikizidi kuhamia kwenye majukwaa ya kidijitali.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika Mkutano wa Mwaka wa Tanzania wa Anwani za Makazi 2026, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Jabir Mohamed, amesema suala la anwani za makazi sasa ni ajenda ya kimkakati ya taifa, hasa katika kipindi hiki cha ukuaji mkubwa wa uchumi wa kidijitali.

Kwa upande wake, akizungumza kwa niaba ya Postmaster Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo, Ferdinand Kabyamela, amesema Mfumo wa Taifa wa Anwani za Makazi umeirahisishia jamii ya wafanyabiashara kujisajili rasmi, kupata huduma za kibenki, mikopo na bima kwa urahisi zaidi.

Hakuna maoni: