Breaking


Jumamosi, 28 Februari 2026

WANAFUNZI WA SEKONDARI ZA NAURA NA MWIVALO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANYAPORI DUNIANI

Kila tarehe 3 mwezi machi Tanzania huadhimisha siku ya wanyama pori Duniani ambapo kwa mwaka huu maadhimisho ya siku hiyo yanafanyika katika Viwanja vya Nanenane Njiro jijini Arusha.

Maadhimisho ya Mwaka huu yanaenda na Kaluli Mbiu “Mimea Dawa, na Manukato: Kutunza Afya, Kuhifadhi Urithi na Kuboresha Maisha” ambapo kabla ya kufikia Kilele tarehe 3 mwezi Machi, shughuli mbalimbali zinaendelea katika viwanja hivyo ikiwemo maonesho ya bidhaa zitokanazo na Mimea Dawa na Manukato lakini pia Maonesho hayo yamejumuisha bidhaa mbalimbali zitokanazo na wanyamapori. 

Kaulimbiu ya mwaka 2026 inaangazia mchango wa mimea dawa, na manukato katika kutunza afya ya binadamu, kudumisha urithi na kuboresha maisha ya jamii. Mimea hii hutumika katika tiba asili na kisasa, na pia ni muhimu katika sekta za vipodozi, vyakula na bidhaa za thamani kubwa, hivyo kuwa na mchango mkubwa kijamii na kiuchumi. Aidha, kimazingira huchangia katika kuimarisha udongo, kuongeza bioanuai na kutoa rasilimali muhimu kwa viumbe wachavushaji kama nyuki na ndege.

Katika kuhakikisha vijana wanashiriki katika maadhimisho hayo Shule za Sekondari Naura na Mwivalo zilishiriki kwa  kufanya mitihani yenye masuala ya Mimea na wanyamapori.

Pia wanafunzi hao walishiriki katika mashindano ya kufukuza kuku, kuvuta  Kamba na kukimbia kwenye magunia. Washindi wa mashindano hayo walipewa zawadi mbalimbali ikiwemo mabegi ya kubebea madaftari, vikombe vya chai, peni na miti kwa shule zao.

Hakuna maoni: