Breaking


Jumatano, 8 Aprili 2026

WATENGENEZA MAUDHUI WAHIMIZWA KUTUMIA AFCON 2027 KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA

 

Watengeneza maudhui mtandaoni jijini Arusha wamehimizwa kutumia kikamilifu fursa ya mashindano ya AFCON 2027 yanayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania, kama jukwaa muhimu la kutangaza vivutio vya utalii na utamaduni wa nchi. 

Wito huo umetolewa na Meneja Mawasiliano wa Tanzania Tourist Board, Pauline Mkama, alipokuwa akichangia mada kuhusu kubiasharisha maudhui ya kitalii, ambapo alisisitiza umuhimu wa kutumia majukwaa ya kidijitali kuinadi Tanzania kimataifa na kuongeza ushindani wa wabunifu wa maudhui.


Aidha, alieleza kuwa mashindano hayo yanaweza kuwa chachu kwa watengeneza maudhui kujipatia soko jipya na kujulikana zaidi duniani, huku yakichangia kukuza sekta ya utalii nchini. Kwa upande wake, mtengeneza maudhui Fahad Rajab alisisitiza umuhimu wa wabunifu kuendelea kujifunza na kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ili kuboresha kazi zao na kubaki na ushindani sokoni.



Naye Magreth Geddy alihimiza matumizi ya teknolojia ya Akili Bandia (AI) katika kuboresha ubora wa maudhui na kuongeza fursa za kibiashara ndani na nje ya nchi. Wito huo unakuja wakati Tanzania ikiendelea na maandalizi ya AFCON 2027, mashindano yanayotarajiwa kuleta manufaa makubwa kiuchumi na kijamii kwa kuvutia wageni wengi na kuongeza utangazaji wa nchi kimataifa.


Hakuna maoni: