Breaking


Jumatano, 8 Aprili 2026

CARDI B ALIPUKA INSTAGRAM BAADA YA KADI YAKE KUPIGWA “DEAL” LA MAMILIONI!


Msanii maarufu wa Hip Hop kutoka Marekani, Cardi B, amewashangaza mashabiki baada ya kulipuka kwa hasira kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Instagram akilalamikia kuibiwa kwa kadi yake ya benki aina ya American Express. Kwa mujibu wa Cardi B, kadi hiyo ilitumika vibaya kufanya manunuzi ya zaidi ya dola 60,000 (zaidi ya shilingi milioni 155 za Kitanzania), jambo lililomfanya ashindwe kuvumilia na kuamua kuweka wazi tukio hilo kwa mashabiki wake.


Katika maelezo yake, Cardi B alifichua kuwa kiasi kikubwa cha fedha hizo kilipotea kwenye maduka ya kifahari, ambapo dola 40,000 zilitumika katika Saks Fifth Avenue huku dola 20,000 zikielekezwa kwenye bidhaa za Apple. Tukio hilo lilimkuta ghafla baada ya kupokea tahadhari za matumizi yasiyo ya kawaida, na bila kupoteza muda aliwasiliana na mhasibu wake kufunga kadi hiyo ili kuzuia hasara zaidi.


Akiwa amejawa na hasira na msisitizo mkubwa, Cardi B aliwaonya hadharani watu anaowashutumu kuhusika na wizi huo, akidai ana ushahidi wa video unaowaonyesha wakitumia kadi yake. Kwa sauti kali na kujiamini, aliwatishia kuwa hawatadumu nje kwa muda mrefu, akisema wazi kuwa wataishia gerezani kabla hata ya wiki kuisha, kauli iliyozua gumzo kubwa mitandaoni na kuwafanya mashabiki kusubiri hatua zitakazofuata.


Hakuna maoni: