Breaking


Jumatano, 8 Aprili 2026

CARRICK APEWA BARAKA OLD TRAFFORD, AMAD ASEMA “NDIYE MTU SAHIHI!”

Winga wa Amad Diallo ameibuka na kauli nzito akimtaja Michael Carrick kuwa ndiye chaguo sahihi kuendelea kuinoa Manchester United kwa kudumu. Kauli hiyo inakuja wakati Carrick akiendelea kufanya vizuri tangu alipochukua mikoba kufuatia kuondoka kwa Ruben Amorim mwezi Januari, ambapo ameiongoza timu kushinda mechi saba kati ya kumi, kupoteza moja pekee na kutoka sare mbili rekodi iliyowasha matumaini mapya kwa mashabiki wa Old Trafford.


Chini ya uongozi wa Carrick, United imeanza kurejea katika ubora wake wa zamani, ikishika nafasi ya tatu kwenye Premier League huku ikiwa na nafasi kubwa ya kufuzu UEFA Champions League msimu ujao. Amad alisisitiza kuwa Carrick anaifahamu vizuri klabu hiyo, ana uzoefu mkubwa na ameweza kujenga uhusiano imara na wachezaji mambo ambayo yanaonekana wazi ndani ya uwanja na nje yake.


Kauli ya Amad imezidi kuchochea mjadala miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka kuhusu mustakabali wa benchi la ufundi la United. Wengi sasa wanaanza kuamini kuwa Carrick si tu kocha wa muda, bali anaweza kuwa suluhisho la muda mrefu la kuirejesha klabu hiyo katika enzi zake za mafanikio makubwa.


Hakuna maoni: