Breaking


Jumamosi, 21 Machi 2026

ACHRAF HAKIMI AKATAA KUPOKEA KOMBE LA AFCON


Mchezaji nyota wa Morocco, Achraf Hakimi, amesema hatopokea kombe la AFCON kufuatia kushindwa kwa timu yake katika mashindano hayo.


Hakimi ameeleza kuwa alishauriwa na mama yake kukataa kupokea kombe hilo, akisisitiza kuwa hana haki ya kulichukua baada ya timu yake kutofanikisha ushindi. Aidha, ametoa wito kwa wachezaji wenzake kufuata msimamo huo.


Amesema Morocco ilikuwa na nafasi ya kushinda, lakini haikufanikiwa, akieleza kuwa huo ndiyo uhalisia wa soka ambapo wakati mwingine unashinda na wakati mwingine unapoteza.


Hakimi ameipongeza Senegal kwa ushindi huo, akieleza kuwa walistahili kutokana na juhudi walizoonyesha uwanjani. Ameongeza kuwa si haki kuharibu furaha yao baada ya mafanikio hayo.


Pamoja na kuheshimu maamuzi ya CAF, Hakimi amesisitiza kuwa hatopokea kombe hilo, akihitimisha kwa kusema kuwa hakushinda AFCON 2025 na kuwatakia pongezi Senegal kwa ushindi wao.


— Achraf Hakimi akizungumza na Marca


Hakuna maoni: