Msemaji wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi ya kiislamu cha Iran, Ali Mohammad Naini, ameuawa katika shambulio.
Shirika la habari la Tasnim, ambalo liko karibu na kikosi hicho maalumu, limeripoti kuwa Jenerali huyo aliuawa katika shambulio ambalo IRGC imezinyoshea kidole cha lawama Israel na Marekani.
Naini alielezewa kama kamanda mkongwe ambaye alikuwa ameitumikia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa zaidi ya miongo minne.
Wakati haya yakiarifiwa, msemaji mkuu wa jeshi la Iran ameonya kuwa mabustani, maeneo ya burudani na sehemu za watalii duniani kote hazitakuwa salama kwa maadui wa Iran.
Jenerali Abolfazl Shekarchi ametoa tishio hilo huku Iran ikiendelea kushambuliwa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni