Breaking


Ijumaa, 27 Machi 2026

DIARRA APIGWA FAINI NA KUFUNGIWA MECHI TATU

 

Bodi ya ligi kuu Tanzania ( TPLB) imemfungia mlinda mlango wa Klabu ya yanga Djigui Diarra kufuatia matukio ya utovu wa nidhamu aliyoonesha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya mtibwa sugar katika dimba la jamhuri Dodoma.

Diarra amekutana na adhabu mbili tofauti ambazo Kwa pamoja analipa faini ya pesa na kukosa michezo.


Adhabu ya Kwanza amefungiwa michezo mitatu na kupigwa faini ya shiling milion mbili ( 2,000,000) Kwa kosa la kumshambulia mwamuzi baada ya kumalizika Kwa mchezo.


 Adhabu ya pili amepigwa faini ya shiling milion mbili ( 2,000,000) Kwa kosa la kuonyesha kidole cha Kati Wakati akitoka uwanjani, kitendo kilichotafsiriwa utovu wa nidhamu.

Hakuna maoni: