Breaking


Ijumaa, 27 Machi 2026

TASAF YAUNGA MKONO SERIKALI UBORESHAJI HUDUMA YA AFYA.

  

Mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF umeunga mkono juhudi za Serikali katika huduma ya afya kwa kutoa msaada muhimu katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.

    Msaada huo umekabidhiwa leo hospitalini hapo na Meneja rasilimali watu wa mfuko huo Mariam Al Jabir kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf Shadrack Mziray.

  Al Jabir ambaye ameambatana na baadhi ya wafanyakazi wa Tasaf amesema  Serikali imewekeza nguvu kubwa katika utoaji wa huduma za afya nchini.

  Aidha baadhi wa Wafanyakazi hao wa Tasaf wakiongozwa na Meneja huyo wamepata nafasi ya kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo huku wakiwafariji kwa kuwatia moyo na kufanya sala fupi kuwaombea uponyaji wa haraka.

Hakuna maoni: