Breaking


Jumapili, 15 Machi 2026

VIJIJI VINNE VYANUFAIKA NA MGAO WA FEDHA ZA WMA MKOANI KATAVI



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 vijiji vinne vimenufaika na mgao wa fedha za Jumuiya ya Wanyamapori (WMA) ya Mpimbwe ambapo Jumuiya hiyo ilipata jumla ya Shilingi 200,000,000/= ambazo ziligawiwa kwenye vijiji vnne vinavyounda Jumuiya hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Katika mgao huo kila kijiji kilipata Shilingi 50,000,000/= ili kutekeleza miradi katika maeneo yao.

Mhe. Chande amebainisha hayo Mkoani Katavi katika mkutano wa hadhara ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba hapa nchini


''Niwahakikishie kwamba mradi huu wa WMA unafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na Wizara itaendelea kufuatilia kwa karibu sana kuhakikisha kwamba wananchi hawa wanapata tija kupitia mradi wa WMA'' amesisitiza Mhe. Chande

Hakuna maoni: