Breaking


Jumapili, 26 Aprili 2026

DC MPOGOLO ATUNUKIWA TUZO MAALUM NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Edward Mpogolo, amepokea Tuzo Maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo,  Severin Mushi, ikiwa ni ishara ya kutambua uongozi wake bora na mchango wake katika kuendeleza sekta ya biashara.


Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala, Edward  Mpogolo amekabidhiwa tuzo hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2026 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), uliofanyika katika Soko Kuu la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, tarehe 25 Aprili 2026.

Hakuna maoni: