Makamu Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Uhamiaji, Said Abeid Kamugisha, amewataka waendeshaji wa mchakato wa usaili wa ajira serikalini kutanguliza maslahi ya Taifa kwa kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na uaminifu katika zoezi la kuwachuja waombaji.
Wito huo umetolewa Aprili 13, 2026, jijini Arusha wakati wa kikao kazi kilicholenga kutoa mwongozo wa uendeshaji wa usaili kwa Vijana walioomba ajira serikali kinachofanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Kamugisha amesisitiza kuwa wataalamu kutoka kada mbalimbali wanapaswa kufanya maamuzi sahihi bila upendeleo wowote, ili kupata watumishi wenye sifa stahiki watakaosaidia kulijenga Taifa.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kufanya maboresho katika sekta ya ajira, ikiwemo matumizi ya mifumo ya kidijitali katika mchakato wa usaili.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni