Breaking


Jumatatu, 13 Aprili 2026

TOENI HUDUMA BORA KWA WALIPAKODI KWA MUJIBU WA SHERIA - CG MWENDA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda amewataka Mameneja wa TRA wa mikoa yote nchini kuendelea kutoa huduma bora kwa walipakodi kwa mujibu wa sheria na kuwa na maamuzi yanayofanana kwa matukio ya kufanana kama sheria zinavyoelekeza.

Kamishna Mkuu Mwenda ametoa maelekezo hayo jijini Mwanza Aprili 13, 2026 alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mameneja wa TRA wa mikoa yote ya kodi kwa nchi nzima kinacholenga kuboresha zaidi utoaji wa huduma za kodi kwa walipakodi kwa upande wa Kodi za ndani na Forodha. 

Akuzungumza katika kikao hicho Kamishna Mkuu amesema kila Meneja katika eneo lake anapaswa kufanya maamuzi ya kikodi kwa kuzingatia sheria ili kuondoa malalamiko ya walipakodi kuhusu kutokutendewa haki katika kutoa maamuzi.

"Nendeni mkaendelee kusimamia sheria za kodi na kutoa maamuzi ya haki kwa walipakodi kwa mujibu wa sheria, siyo unatoa maamuzi ambayo hayalingani na sheria zinavyotaka, inatakiwa maamuzi ya Mwanza yaendane na maamuzi ya Ilala na maamuzi ya Mtwara, hii itaongeza zaidi imani ya walipakodi kwa taasisi" amesema Bw. Mwenda.

Amewahakikishia walipakodi wote nchini kuwa watapata huduma bora na za kufanana bila kujali wapo katika mikoa gani maana TRA ni moja na inafanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Hakuna maoni: