SEHEMU YA 1: NDOTO ISIYOONEKANA KWA MACHO
Katika kijiji kidogo kilichozungukwa na kelele za soko na harufu ya mbao zilizochongwa, aliishi kijana aitwaye Baraka. Tofauti na vijana wengine, Baraka hakuweza kuona alizaliwa bila uwezo wa kuona dunia kwa macho yake.
Lakini ndani yake, kulikuwa na ndoto kubwa isiyoonekana kwa macho, bali iliyojaa mwanga wa matumaini.
Tangu akiwa mdogo, alipenda kusikiliza sauti za vitu hasa tik-tik za saa. Kwa wengine ilikuwa kelele ya kawaida, lakini kwa Baraka ilikuwa muziki wa ajabu uliomvutia kila siku.
Wakati watoto wengine wakicheza, yeye alikuwa karibu na fundi saa wa kijijini, akisikiliza kwa makini kila sauti ndogo iliyotoka kwenye saa zilizokuwa zikirekebishwa.
Siku moja, alimwambia mama yake:
“Mama, siku moja nitatengeneza saa bora zaidi duniani.”😋😋
Mama yake alitabasamu kwa huzuni, akijua ugumu wa ndoto hiyo.😊😔
Lakini Baraka hakujali. Ndoto yake ilikuwa hai.
(Itaendelea – Sehemu ya 2: Mwanzo wa Safari Ngumu)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni