Msanii maarufu wa Nigeria, Davido, amewahi kufunguka kwa staili ya kusisimua kuhusu mwanzo wa penzi lake na mke wake, Chioma Avril Rowland, akieleza kuwa kila kitu kilianza kama filamu ya mapenzi chuoni Babcock University. Davido anasema alimvutia Chioma mara ya kwanza alipomuona akitembea kwa kujiamini, kitu kilichomfanya achukue hatua ya haraka kwa kumtuma rafiki yake Lati kwenda kumuita lakini mambo hayakwenda kama alivyotarajia kwani hakupata majibu yoyote papo hapo.
Akiendelea kusimulia kwa hisia na vicheko, Davido alikumbuka tukio hilo kwa kusema kuwa kipindi hicho alikuwa ametoka kuachia hit yake kubwa “Damiduro,” na alikuwa ndani ya gari lake aina ya Prado alipomuona Chioma kwa mara ya kwanza. Licha ya juhudi zake za mwanzo kugonga mwamba, hakukata tamaa, kwani hatimaye walikutana tena jijini Lagos ambapo ndipo aliamini kabisa kuwa bahati yake ya mapenzi ilikuwa imefika.
Hadithi hii ya mapenzi inaonesha wazi kuwa wakati mwingine mapenzi huanza kwa jaribio moja tu la ujasiri na subira kidogo. Kutoka kutopata jibu hadi kusema “Nimekupata,” safari ya Davido na Chioma ni ushahidi kuwa penzi la kweli linaweza kuchanua kwa namna isiyotarajiwa na leo hii wawili hao ni moja ya couple zinazovutia zaidi kwenye ulimwengu wa burudani Afrika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni