Breaking


Jumanne, 7 Aprili 2026

MVUA KUBWA KUTARAJIWA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI NDANI YA SAA 24 ZIJAZO

 Mamlaka ya hali ya hewa imetoa tahadhari ya uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika saa 24 zijazo, hususan katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Lindi, Mtwara na Pwani ikiwemo visiwa vya Mafia, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo, ikiwemo mafuriko ya ghafla na usumbufu wa miundombinu. 


Aidha, wavuvi na wasafiri wa majini wameshauriwa kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuepuka safari zisizo za lazima katika kipindi hiki ili kuhakikisha usalama wao.


Hakuna maoni: