Breaking


Jumanne, 7 Aprili 2026

OFFSET APIGWA RISASI NDANI YA CASINO FLORIDA


Rapa maarufu Offset ameripotiwa kupigwa risasi akiwa katika casino moja huko Hollywood, Florida nchini Marekani, tukio lililotokea usiku wa Jumatatu Aprili 6 majira ya saa 1 kamili. Kwa mujibu wa taarifa za awali, msanii huyo alikuwa katika eneo la maegesho ya valet karibu na Seminole Hard Rock Hotel & Casino wakati tukio hilo lilipotokea, hali iliyozua taharuki kwa mashuhuda waliokuwepo eneo hilo.


Msemaji wa Offset amethibitisha kupitia jarida la XXL kuwa rapa huyo yuko katika hali nzuri baada ya kukimbizwa hospitali ya karibu kwa matibabu ya haraka. Aidha, kwa mujibu wa taarifa kutoka TMZ, Idara ya Polisi ya Seminole imekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kuanza uchunguzi wa kina kubaini chanzo na wahusika wa shambulio hilo.


Ripoti zaidi zinaeleza kuwa watu wawili tayari wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo, huku mamlaka zikiahidi kutoa taarifa zaidi kadri uchunguzi unavyoendelea. Tukio hili limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa muziki na wadau wa burudani duniani, wengi wakionesha wasiwasi juu ya usalama wa wasanii katika maeneo ya umma.


Hakuna maoni: