Breaking


Alhamisi, 23 Aprili 2026

REA IMELETA MAGEUZI SEKTA YA NISHATI

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii maeneo ya Vijijini kupitia miradi ya Usambazaji Umeme na uhamasishaji na uwezeshaji wa Teknolojia zilizoboreshwa za Nishati Safi ya Kupikia kwa wananchi kote nchini.

Hayo yameelezwa Aprili 23, 2026 na Mbunge wa Sikonge ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhe. Amos Maganga.

"Ninawapongeza sana REA, mnafanya kazi kubwa, miradi mliyotekeleza kote nchini imechagiza ukuaji wa uchumi Vijijini lakini pia imeboresha huduma za Jamii katika maeneo hayo," amebainisha Maganga.

Amesema kwa sasa hakuna tofauti kati ya vijiji na miji kwani kupitia miradi iliyotekelezwa na REA huduma muhimu ikiwemo za afya na elimu kote zinapatikana kwa ubora sawa.


Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti, Wabunge waliotembelea Banda la REA walimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy kwa uongozi wake ambao walisema umeleta chachu kwenye utekelezaji wa miradi.

Hakuna maoni: