Breaking


Jumapili, 12 Aprili 2026

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO


Mamlaka ya Hali ya hewaTanzania imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa Aprili 12, 2026, ikieleza kuwa maeneo mengi nchini yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi yakichanganyika na vipindi vya jua pamoja na mvua za hapa na pale. 


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mikoa ya pwani ikiwemo Dar es Salaam na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba itashuhudia mvua katika maeneo machache, huku maeneo ya magharibi na kanda ya ziwa yakipata hali kama hiyo. 


Aidha, tahadhari imetolewa kuwa kuna uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa kuambatana na ngurumo katika baadhi ya maeneo ya kaskazini hususan Kilimanjaro, Arusha  na Manyara , hivyo wananchi wanashauriwa kuchukua tahadhari stahiki.


Hakuna maoni: