Breaking


Jumatatu, 18 Mei 2026

DROO YA AFCON 2027 TANZANIA, UGANDA NA KENYA KUCHEZESHWA NA MAGWIJI WA SOKA AFRIKA


Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza kuwa droo ya michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika 2027 (AFCON 2027) itachezeshwa na baadhi ya magwiji wa soka barani Afrika akiwemo Max-Alain Gradel, William Troost-Ekong, Essam El Hadary pamoja na Trésor Mputu.

Droo hiyo muhimu kwa mataifa yatakayoshiriki safari ya kuelekea AFCON 2027 inayotarajiwa kufanyika kwa ushirikiano wa Tanzania, Uganda na Kenya, itafanyika Jumanne Mei 19, 2026 katika ofisi za Egypt Football Association jijini Cairo, Misri.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, hafla hiyo ya droo itaanza saa tisa alasiri kwa saa za Afrika Mashariki huku ikipewa uzito mkubwa kutokana na maandalizi ya michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika. Mashabiki wa soka wanatarajia kufahamu makundi yatakayoundwa pamoja na ratiba ya mechi za kufuzu.

AFCON 2027 itakuwa historia kwa ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Tanzania, Uganda na Kenya kupata nafasi ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa pamoja. Hatua hiyo imeelezwa kuwa fursa muhimu ya kukuza soka, utalii na uwekezaji katika nchi hizo tatu.


Hakuna maoni: