Breaking


Jumatatu, 18 Mei 2026

GRIEZMANN AOMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI WA ATLETICO MADRID BAADA YA KUJIUNGA BARCELONA

Kiungo mshambuliaji wa Atlético Madrid, Antoine Griezmann, ameomba radhi kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na uamuzi wake wa zamani wa kuondoka na kujiunga na FC Barcelona, akieleza kuwa wakati huo alikuwa bado kijana na hakuelewa thamani ya mapenzi aliyokuwa akionyeshwa na wapenzi wa Atlético Madrid.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amesema baada ya kuondoka Atlético Madrid ndipo alipogundua umuhimu wa mahusiano yake na mashabiki wa klabu hiyo, hali iliyomfanya kufanya juhudi kubwa kurejea tena katika timu hiyo ili kuendelea kufurahia soka pamoja na sapoti ya mashabiki.

“Ninaomba mnisamehe, nilikuwa kijana na nilifanya makosa kujiunga na Barcelona. Wakati huo sikuuelewa upendo niliokuwa nao hapa. Baadaye nilitambua kosa langu na nilifanya kila kitu ili nirejee tena na kufurahia kuwa hapa,” alisema Griezmann.

Mchezaji huyo mwenye uzoefu mkubwa pia amesema kuwa licha ya kushindwa kutwaa mataji makubwa kama La Liga na UEFA Champions League akiwa Atlético Madrid, bado anaamini upendo kutoka kwa mashabiki ndiyo mafanikio makubwa zaidi katika maisha yake ya soka.

“Sikushinda La Liga wala UEFA Champions League, lakini upendo wenu ndiyo kitu muhimu zaidi kwangu,” aliongeza Griezmann.

Kauli hiyo imeibua hisia mbalimbali kwa mashabiki wa Atlético Madrid, wengi wao wakionesha kuendelea kumpokea kwa moyo mmoja kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya klabu hiyo kwa miaka tofauti.


Hakuna maoni: