Kupunguzwa kwa tozo hiyo kunatajwa kuwa mafanikio muhimu kwa sekta binafsi, yaliyotokana na majadiliano kati ya Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Wizara ya Uchukuzi. Ushirikiano huo umeelezwa kuwa mfano mzuri wa jitihada za pamoja kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuboresha mazingira ya biashara nchini.
Wadau wa biashara wanaamini hatua hiyo itasaidia kuongeza ushindani wa bidhaa sokoni, kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya biashara na usafirishaji.
Kutokana na mabadiliko hayo, wafanyabiashara wamehimizwa kupitia upya makadirio yao ya gharama za uagizaji, bajeti pamoja na mifumo ya upangaji bei ili kuendana na kiwango kipya cha tozo kitakachoanza kutumika rasmi mwezi Julai mwaka huu.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni