Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Lazaro Twange ameeleza kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayetekeleza mradi wa maboresho ya Kituo cha Kufua Umeme cha Hale kutokana na kuchelewa kukamilika kwa Mradi huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2022.
Twange ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika mradi wa Hale pamoja na mradi wa usafishaji wa bwawa la Mto Pangani iliyopo katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo amemtaka mkandarasi wa Mradi wa Hale kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kuongeza wafanyakazi pamoja na muda wa kufanya kazi ili ukamilike kwa wakati.
Amesema mradi huo una maeneo saba ya utekelezaji ambapo maeneo mawili tayari yamekamilika huku mengine yakiendelea na utekelezaji.
Aidha, kuhusu mradi wa usafishaji wa bwawa la Pangani, Twange amesema matarajio ya TANESCO ni kuhakikisha kazi hiyo inakamilika ndani ya muda uliopangwa ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu wa mvua.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni