WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema serikali inaendelea na jitihada za kuboresha Sheria ya Elimu ili iweze kuendana na mahitaji na mabadiliko ya sasa katika sekta ya elimu nchini.
Kutokana na hilo amewataka wadau wa elimu nchini kuhakikisha mchakato wa ukusanyaji wa maoni kuhusu sera na sheria ya elimu unakamilika kwa wakati ili kuwezesha utekelezaji wa malengo yaliyowekwa na Serikali.
Prof.Mkenda ameyasema hayo Mei 21,2026 jijini Dodoma wakati akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353.
Amesema tayari sera mpya ya elimu imezinduliwa na hatua inayofuata ni kufanya maboresho ya sheria ili kuendana na mwelekeo huo mpya wa elimu ifikapo mwaka 2028.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir,amesema kuwa mchakato huo umechukua muda mrefu kwa lengo la kuhakikisha inapatikana sheria inayozingatia maoni ya wananchi wengi na wadau wa elimu.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni