Zaidi ya Waandishi wa habari na Watangazaji 40 wanaoandika na kutangaza vipindi vya watoto malezi, matunzo ya mtoto na familia, kuhusu wajibu wa Wazazi na walezi katika malezi na matunzo ya familia, wamekiri kuiva kuwa vinara.
Mafunzo hayo ya siku tano, yaliyofanyika jijini Dar es salaam, yameshirikisha waandishi wa habari kutoka Mikoa mbalimbali, yamewajengea uwezo wa kuboresha vipindi na habari ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Akizungumza wakati wa ufungaji Mafunzo hayo, Mwezeshaji wa Kifatifa kuhusu masuala ya Kijinsia, kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum Victor Lubaragamu, amesema matumaini makubwa kwa kundi lililopata mafunzo hayo kwenda kuyafanyia kazi na kuleta matokeo chanya.
Jambo lililoungwa Mkono, na Mwezeshaji mwingine wa Kitaifa katika masuala ya Kupinga Ukatili, Sabrina Majtaka, kwa kuwataka waandishi na Watangazaji kuandaa vipindi na kuandika habari kwa kufuata miiko ya uandishi pindi wanaporipoti habari za ukatili hasa za Watoto.
Kwa upande wao waandishi wa habari na watangazaji, wamekiri kuiva na kuwa tayari kalamu na sauti zao kueleza dhana ya familia bora, ijengwe kupitia misingi ya kitamaduni ya malezi ya watoto kwa kuzingatia vipengele muhimu ikiwemo Kumjali, Kumlinda na Kuzungumza nae.
Mafunzo hayo ya siku tano yamegusia mada juu ya suala la lishe, Ulinzi wa Mtoto, Umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa, kuwajali kina mama na watoto wenye ulemavu, kukabiliana na VVU na Ukimwi, na kuwajali vijana balehe.
Waandishi na Watangazaji Vinara, linakua kundi la tatu kupatiwa mafunzo hayo chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa linalohusika na kulinda haki, kuboresha afya, elimu na ustawi wa watoto na wanawake duniani ( Unicef) kwa kuwezesha mafunzo hayo ya siku tano.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni