Kwa mujibu wa Cucurella, ameamua kutokuzikata nywele zake ili kumrahisishia mwanawe, Mateo, ambaye anaishi na hali ya autism, kumtambua kwa urahisi anapokuwa akicheza mbele ya maelfu ya mashabiki uwanjani. Hatua hiyo humsaidia mtoto wake kupunguza msongo na wasiwasi unaoweza kujitokeza katika mazingira yenye kelele na umati mkubwa wa watu.
Mchezaji huyo amesema uamuzi huo umetokana na upendo wake kwa familia, akiamini kuwa jambo hilo dogo lina mchango mkubwa katika kumfanya mwanawe ajisikie salama na mwenye utulivu wakati wa kushuhudia mechi.
Hadithi ya Cucurella imepokelewa kwa hisia chanya na mashabiki wengi wa soka duniani, ikionyesha kuwa nyuma ya mafanikio ya wanasoka maarufu kuna simulizi za maisha zinazogusa mioyo. Tukio hilo pia linaendelea kuongeza uelewa kuhusu autism na umuhimu wa msaada wa familia kwa watoto wanaoishi na hali hiyo.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni