Katika Kombe la Dunia la mwaka huu, mshambuliaji huyo alifunga mabao nane, akivunja rekodi ya mabao ya mchezaji wa Ufaransa katika toleo moja la Kombe la Dunia. Aidha, amefikisha jumla ya mabao 20 katika historia ya ushiriki wake kwenye Kombe la Dunia akiwa bado na umri wa miaka 27, jambo linalomweka miongoni mwa washambuliaji waliofanikiwa zaidi katika historia ya mashindano hayo.
Baada ya kumalizika kwa safari ya Ufaransa, Mbappé aliwashukuru mashabiki kwa sapoti yao isiyoyumba, huku akisisitiza kuendelea kuwajibika kama kiongozi wa timu na kuangazia malengo ya baadaye.Licha ya kuondolewa kwenye mashindano, kiwango cha Mbappé kimeendelea kuvutia wadau wengi wa soka duniani, huku wengi wakimpongeza kwa uongozi, kujituma na mchango wake mkubwa kwa timu ya taifa ya Ufaransa.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni