Breaking


Jumapili, 30 Agosti 2026

MAUA SAMA AONYESHA UJAUZITO WAKE KWA MARA YA KWANZA

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Maua Sama, ameonekana kwa mara ya kwanza hadharani akionyesha ujauzito kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kwa muda, taarifa kuhusu ujauzito wa msanii huyo zimekuwa zikizungumzwa kwenye mitandao ya kijamii, lakini sasa Maua Sama ameweka wazi hatua hiyo mpya ya maisha yake kupitia picha aliyoishirikisha na mashabiki wake.

Katika ujumbe wake, Maua Sama ameandika “Am grateful, Alhamdulillah”, akieleza shukrani zake katika hatua hiyo muhimu.

Ujumbe huo umeibua hisia za furaha miongoni mwa mashabiki, wasanii wenzake na wadau mbalimbali wa burudani ambao wamejitokeza kumpongeza kwa hatua hiyo.

Hata hivyo, Maua Sama hajaeleza wazi iwapo tayari amejifungua au bado anaendelea na safari ya ujauzito, hivyo taarifa zaidi kuhusu hilo zitasubiri uthibitisho kutoka kwake mwenyewe.

Madelemo News inamtakia Maua Sama kila la heri katika hatua hii mpya ya maisha.

💬 Ujumbe wako wa pongezi kwa Maua Sama ni upi?


Hakuna maoni: