Breaking


Alhamisi, 27 Agosti 2026

REAL MADRID YAMSAJILI BEKI CHIPUKIZI OSCAR NAASEI



Madrid, Hispania 


Real Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili beki wa kati mwenye umri wa miaka 21, Oscar Naasei, katika usajili unaolenga kuendeleza vipaji vya vijana ndani ya klabu hiyo.

Naasei, raia wa Ghana, amekamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa muda mrefu na Real Madrid. Kwa mujibu wa taarifa za usajili huo, Granada inatarajiwa kupokea ada ya takribani euro milioni 2.

Beki huyo anachukuliwa kuwa mchezaji mwenye uwezo wa kuja kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Real Madrid hapo baadaye. Hata hivyo, kwa hatua ya awali, Naasei atajiunga na Real Madrid Castilla, timu ya pili ya klabu hiyo, ili kupata uzoefu na kuendelea kuimarisha uwezo wake.

Usajili huo unaendana na mkakati wa Real Madrid wa kuwekeza katika wachezaji vijana wenye kipaji na kuwaendeleza kwa ajili ya kikosi cha kwanza.

Je, unauonaje usajili wa Oscar Naasei? Unaupa alama ngapi kati ya 1 hadi 10?


Hakuna maoni: