Breaking


Alhamisi, 13 Agosti 2026

TREY SONGZ AWASILI TANZANIA KWA AJILI YA TAMASHA LA IMBEJU SAUTI MOJA

Msanii maarufu wa muziki wa R&B kutoka Marekani, Trey Songz, amewasili nchini Tanzania usiku wa kuamkia Agosti 13, 2026, kwa ajili ya kutoa burudani katika tamasha la Imbeju Sauti Moja.


Trey Songz anatarajiwa kupanda jukwaani
Agosti 14, 2026, katika Kijitonyama Postal Grounds, Dar es Salaam, ambapo mashabiki watapata fursa ya kushuhudia burudani kutoka kwa msanii huyo wa kimataifa.

Kwa mashabiki ambao bado hawajakata tiketi, bado kuna nafasi ya kuwa sehemu ya tukio hilo. Bei za tiketi ni:

  • Tiketi ya kawaida: TZS 50,000
  • VIP: TZS 130,000
  • Meza: Nafasi chache bado zinapatikana

Tamasha hilo linatarajiwa kuwa sehemu ya matukio makubwa ya burudani jijini Dar es Salaam, likiwakutanisha mashabiki wa muziki na burudani kutoka maeneo mbalimbali.

Trey Songz Tanzania — The Wait Is Over.

Wikiendi moja. Jukwaa moja. Sauti Moja.


Hakuna maoni: