Msanii wa muziki kutoka Marekani, Ciara, anatarajia mtoto mwingine, ikiwa ni ujauzito wake wa tano na mtoto wake wa nne na mume wake, Russell Wilson.
Ciara na Russell Wilson, ambao wameoana tangu mwaka 2016, walitangaza taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii kwa kushiriki video ikimuonyesha Ciara akitundika fulana nyeupe zinazowakilisha kila mmoja wa wanafamilia pamoja na mtoto anayetarajiwa.
Habari hiyo imepokea pongezi kutoka kwa mashabiki na watu mbalimbali, huku wengi wakifurahishwa na hatua mpya katika maisha ya familia ya Ciara na Russell Wilson.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni