Breaking


Jumatatu, 7 Septemba 2026

UZINDUZI WA MAJENGO NA BARABARA MTUMBA WAAHIRISHWA



Dodoma:


Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) imetangaza kuahirishwa kwa hafla ya uzinduzi wa majengo ya Wizara, Taasisi za Serikali pamoja na barabara za lami katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Hafla hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika Jumanne, Septemba 8, 2026, lakini imeahirishwa hadi tarehe nyingine ambayo itatangazwa rasmi na mamlaka husika.

Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa taarifa hiyo kwa umma na kuwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa rasmi kuhusu tarehe mpya ya kufanyika kwa hafla hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu).


Hakuna maoni: