Breaking


Jumanne, 8 Septemba 2026

CLATOUS CHAMA AJIBU MJADALA MITANDAONI, ASEMA “NINA UKWELI NA USHAHIDI”



Mchezaji wa soka Clatous Chama ametoa kauli kupitia mitandao ya kijamii, akieleza kutoridhishwa na baadhi ya mijadala na maoni yanayoendelea kuhusu yeye.

Chama amesema amekuwa kimya kwa muda, lakini anaona baadhi ya watu wameanza kuvuka mipaka. Ameeleza kuwa mitandao ya kijamii ina nafasi ya watu kutoa maoni, huku akisisitiza kuwa ukweli unatakiwa kutofautishwa na kauli zinazotolewa kwa lengo la kutafuta umaarufu, likes au maoni.

Katika ujumbe wake, Chama amesema anaamini katika kusimamia ukweli na kwamba ana ushahidi wa mambo anayoyazungumzia. Pia ameeleza kuwa yuko tayari kuendelea kujibu mjadala huo iwapo utaendelea.

Chama amehoji pia sababu ya podcast yake kuonekana kuibua mjadala, huku akisema kuwa endapo kutakuwa na machapisho mengine yanayomhusu, anaweza kuweka hadharani mawasiliano mbalimbali anayodai kuwa nayo.

Kauli hiyo imekuja wakati mjadala ukiendelea kwenye mitandao ya kijamii, huku Chama akisisitiza kuwa yuko tayari kueleza upande wake kuhusu suala hilo.

 

Hakuna maoni: