Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limeona picha mjongeo inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana anayejitambulisha kwa jina la Giles George Nandi wa Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa akiwa amefungwa pingu na akidai kwamba amekuwa nazo kwa muda wa siku tatu bila sababu.
Jeshi la Polisi baada ya kuiona picha hiyo mjongeo linafanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidı kubaini askari aliyefanya kitendo hicho ili hatua za haraka zichukuliwekulingana na ukiukwaji wa sheria utakaobainika, kwani hakuna aliye juu ya sheria.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Rukwa.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni