Breaking


Alhamisi, 24 Septemba 2026

KARIAKOO LAZIMA IPITIKE - CHALAMILA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Arbelt Chalamila, amefanya ziara ya kutembelea mitaa mbalimbali ya kata ya Kariakoo kuangalia na kujiridhisha hali ya Usafi katika Soko Kuu la Kimataifa Kariakoo.


Akikagua maeneo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Arbelt Chalamila, amewataka wafanyabiasha wanaoshusha mizigo katikati ya Soko wanatakiwa kushusha nje kulingana na maagizo ya awali yaliyotolewa.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao, na  Viongozi alioambatana nao,  Chalamila, amesema Soko la Kariakoo linategemewa na watu mbalimbali hivyo ni vema njia za Soko zikapitika.


Awali Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es salaam, amepokea taarifa ya Usafi ya  Jiji la Dar es salaam,  mara baada  ya agizo la Rais Dokta Samia Suluhu Hassan, kuwataka Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha Jiji linakua safi.

Ambapo taarifa hiyo imeeleza hatua walizochukua kuhakikisha Usafi unafanyika, kufungua njia na uzibuaji wa mitaro inayopitosha Maji hasa kuelekea katika msimu wa Mvua zinatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Hakuna maoni: