Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki ufunguzi rasmi wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yaliyozinduliwa tarehe 26 Septemba, 2026 na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo *Mhe. Paul Christian Makonda* Mkoani Kilimanjaro.
Mashindano hayo yalianza tarehe 23 Septemba, 2026 yakiwahusisha Watumishi wa Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Akiwakilisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu *Bi. Faith Minani* aliwapongeza Watumishi kwa juhudi wanazoonesha katika Mashindano ya SHIMIWI.
*"Kwa niaba ya Viongozi wetu na menejimenti kwa ujumla, nawapongeza sana Watumishi wenzangu kwa jitihada mnazoonesha katika Mashindano haya, tunatarajia ushindi kutoka kwenu"* Amesema Bi. Faith Minani
Nae Mwenyekiti wa Michezo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Felix Mshama ameushukuru Uongozi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kutoa kipaumbele katika michezo ambayo itawasaidia kuimarisha Afya na kudumisha mahusiano baina ya Watumishi.
Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2026 yanafanyika Mkoani Kilimanjaro yamezinduliwa rasmi tarehe 26 Septemba, 2026. Mashindano hayo yataendelea hadi tarehe 7 Oktoba, 2026 katika Viwanja mbali mbali vya michezo vilivyopo mjini Moshi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni