Kiongozi wa Sekta Binafsi Tanzania na Mmiliki wa Bravo Group na Agricom, Bi. Angelina Ngalula, amefikisha salamu za pole na rambirambi kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kufuatia msiba wa kuondokewa na mwenza wake mpendwa, Mhe. Maalim Hafidh Ameir Hassan
Bi. Ngalula alifika kwa niaba ya Sekta Binafsi Tanzania, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa TPSF, kuwasilisha pole kwa niaba ya wadau wote wa Sekta Binafsi walioshindwa kufika binafsi
Tunamuomba Mwenyezi Mungu amuweke Marehemu mahali pema peponi, na awape Mhe. Rais, familia na ndugu wote subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi.
*Innā lillāhi wa innā ilayhi rājiʿūn. 🇹🇿*
#TPSF #SektaBinafsiTanzania #SalamuZaPole #Rambirambi



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni