Mshambuliaji wa pembeni, Simon Adingra, amejiunga na Ajax kwa mkataba wa mkopo akitokea Sunderland, katika dili ambalo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya euro milioni 3 kwa awamu ya awali.
Kwa mujibu wa taarifa za usajili huo, Ajax imepewa kipengele cha kumnunua moja kwa moja Adingra baada ya kumalizika kwa kipindi cha mkopo. Kipengele hicho kina thamani ya takribani euro milioni 16.
Adingra tayari amefanyiwa vipimo vya afya (medical) na Ajax, hatua inayofungua njia ya kukamilishwa rasmi kwa uhamisho wake.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Ajax, huku klabu hiyo ikitazama uwezekano wa kumfanya kuwa sehemu ya kikosi chake kwa muda mrefu endapo atafanya vizuri katika kipindi cha mkopo.
Usajili huo unatarajiwa kuwa sehemu ya mipango ya Ajax ya kuimarisha kikosi chake kwa msimu mpya wa mashindano.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni