Breaking


Jumamosi, 5 Septemba 2026

TAMASHA LA NYANGUMI LAFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI MTWARA


Tamasha la Nyangumi linalofanyika mkoani kuanzia Septemba 02-05 mkoani Mtwara limeanza kufungua fursa za kiuchumi ambapo wadau mbalimbali wa sekta binafsi wameonesha nia ya kuchangamkia fursa hizo.




Hayo yamebainika Septemba 04,2026  wakati wa kongamano lililofanyika kando ya tamasha hilo ambalo limekutanisha wadau hao kutoka mashirika yasiyo na kiserikali, Taasisi za kifedha,Vyombo vya habari na wawekezaji binafsi ambapo wameainisha fursa kadhaa zinazoambatana na uwepo wa Tamasha la nyangumi ikiwa ni pamoja na ajira kwa vijana wenye vyombo vya usafiri hususan mitumbwi inayopelekea watalii kushuhudia tukio hilo na nyumba za kulala wageni hao.

Hakuna maoni: