Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha, amekutana na waandishi wa habari na kueleza kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 46 wa wakuu wa Mamlaka za Kodi za Jumuiya ya Madola (Commonwealth Association of Tax Administrators – CATA) utakaofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2026, ukiwakutanisha washiriki kutoka mataifa 48.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Mcha amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa Tanzania kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika usimamizi wa kodi, kubadilishana uzoefu na mbinu bora za ukusanyaji wa mapato, pamoja na kujifunza mikakati ya kisasa ya kuongeza ufanisi katika usimamizi wa kodi.
Aidha, amesema mkutano huo utaipa Tanzania fursa ya kuonesha uwezo wake wa kuandaa na kuendesha mikutano ya kimataifa, kukuza utalii na biashara kupitia ujio wa washiriki kutoka mataifa mbalimbali, pamoja na kuimarisha nafasi ya Tanzania katika mijadala ya kimataifa kuhusu usimamizi wa kodi na maendeleo ya uchumi.
TRA itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa taarifa sahihi kuhusu mkutano wa CATA 2026 na fursa zinazotokana na mkutano huo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uelewa wa wananchi, uwazi na kuitangaza Tanzania katika jukwaa la kimataifa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni