Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo, kuanzia saa 3:00 usiku wa leo, Septemba 6, 2026.
Kwa mujibu wa utabiri huo, maeneo mbalimbali nchini yanatarajiwa kuwa na hali tofauti za hewa, ikiwemo mawingu kiasi, vipindi vya jua pamoja na mvua nyepesi katika baadhi ya maeneo.
Utabiri kwa maeneo mbalimbali
Mkoa wa Tanga: Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Visiwa vya Unguja na Pemba: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dodoma na Singida: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mkoa wa Pwani, ikijumuisha Visiwa vya Mafia: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Lindi na Mtwara: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Shinyanga na Simiyu: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Songwe, Ruvuma, Iringa na Njombe: Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa taarifa na tahadhari zaidi kadiri zinavyotolewa.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni