Breaking


Jumatatu, 26 Oktoba 2026

RAIS SAMIA AMPONGEZA RAIS LULA WA BRAZIL BAADA YA KUCHAGULIWA TENA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa pongezi kwa Rais Luiz Inácio Lula da Silva wa Jamhuri ya Shirikisho la Brazil kufuatia kuchaguliwa kwake tena kuwa Rais wa nchi hiyo.

Katika ujumbe wake, Rais Samia ameeleza kuwa Tanzania inathamini urafiki wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na Brazil, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa mataifa hayo mawili.

Amesema Tanzania inaangalia mbele katika kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia na kupanua maeneo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania na Brazil.

Aidha, Rais Samia amemtakia Rais Lula mafanikio katika kipindi chake kipya cha uongozi, pamoja na kuwatakia wananchi wa Brazil kuendelea kufurahia amani na ustawi.

Ujumbe huo unaonesha dhamira ya Tanzania ya kuendeleza urafiki na ushirikiano wa kimataifa, hususan katika kujenga uhusiano wenye manufaa kwa mataifa yote mawili.

Chanzo: Ujumbe wa pongezi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Hakuna maoni: