Breaking


Alhamisi, 15 Oktoba 2026

TCRA YAWAPA SIKU 30 WATOA HUDUMA ZA INTANETI KUREKEBISHA NYAYA HOLELA

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania-TCRA, imewapa watoa huduma za intaneti siku 30 za kurekebisha nyaya holela zilizowekwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, hatua inayolenga kuimarisha usalama wa wananchi na kuboresha mandhari ya Jiji.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, EDWARD MPOGOLO, tarehe 10 Oktoba mwaka huu, kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, ELIHURUMA MABELYA, kuiandikia TCRA barua kuhusu uwepo wa nyaya hizo. 

Agizo hilo lilitolewa mara baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi.

Utekelezaji wa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi na salama kwa kuondoa nyaya zinazoweza kuhatarisha wananchi na kuhakikisha miundombinu ya mawasiliano inawekwa kwa kuzingatia taratibu zinazofaa.

Hakuna maoni: