Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amezindua Ripoti ya Utendaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) Tanzania ya mwaka 2025, leo Oktoba 15, 2026
Ripoti hiyo inalenga kuonesha hali ya maendeleo ya SACCOS nchini na mchango wake katika kukuza uchumi wa wananchi kupitia huduma za kifedha, upatikanaji wa mikopo na kuimarisha utamaduni wa kuweka akiba.
Uzinduzi wa ripoti hiyo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya ushirika nchini, ambayo ina nafasi muhimu katika kuwawezesha wananchi kupata huduma za kifedha na kuchochea shughuli za kiuchumi.
Ripoti hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 26 la Vyama vya Akiba na Mikopo Barani Afrika (2026 SACCA Congress).






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni