Breaking


Alhamisi, 5 Novemba 2026

KANYE WEST AONEKANA PAMOJA NA WATOTO WAKE KATIKA MAONESHO YA MITINDO YA YEEZY


Rapa maarufu Kanye West ameonekana akiwa na furaha pamoja na watoto wake wanne, North, Saint, Chicago na Psalm, katika tukio la maonesho ya mitindo ya mavazi ya chapa yake ya Yeezy.

Tukio hilo lilifanyika jana usiku katika jengo la Yeezy Flagship Droam 1 lililopo Los Angeles, Marekani, ambapo Kanye aliandaa maonesho ya mavazi ya Yeezy Season 01.


Picha kutoka katika tukio hilo zimemuonyesha msanii huyo akiwa pamoja na watoto wake, jambo lililovutia hisia za mashabiki na wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii.

Maonesho hayo ni sehemu ya shughuli za Kanye West katika kukuza chapa yake ya mitindo ya Yeezy, ambayo imeendelea kutambulika katika tasnia ya mavazi na mitindo duniani.

Chanzo: Taarifa ya tukio la Yeezy Season 01.


Hakuna maoni: