Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekamilisha maandalizi ya awali ya mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Morogoro hadi Dumila, wenye urefu wa kilomita 66, pamoja na ujenzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha 220/33kV katika eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Sara Msafiri Ally, aliyetaka kujua lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo hicho na laini ya umeme, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema kuwa hatua inayofuata ni kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Aidha, Makamba ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo umepangwa kuanza baada ya kukamilika kwa miradi ya awamu ya kwanza ya Gridi Imara.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni