Breaking


Jumatano, 4 Novemba 2026

WAMAREKANI WANATAKA SIASA ZA KUWAUNGANISHA BADALA YA KUWAGAWA-OBAMA



Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, amesema matokeo ya uchaguzi wa katikati ya muhula nchini humo, yanaonesha kuwa Wamarekani wanataka siasa zinazowaunganisha badala ya kuwagawa, pamoja na viongozi wanaotoa suluhisho la changamoto zinazowakabili.


Katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Obama, amesema ushindi huo umechangiwa na wagombea waliojitokeza kuwania nafasi za uongozi katika maeneo mbalimbali nchini humo, yakiwemo maeneo yaliyokuwa yakichukuliwa kuwa ngumu kwa Democrat kushinda. 


Licha ya utawala wa sasa kubakiza miaka miwili madarakani, amesema jukumu la chama chake kwa sasa ni kufanya mabadiliko katika maeneo wanayoweza, kuzuia madhara zaidi na kuweka msingi wa mustakabali wa taifa hilo.

Katika uchaguzi huo, Chama cha Democrat kimefanikiwa kupata udhibiti wa Seneti na Bunge la Wawakilishi la Marekani, hatua inayokipa mamlaka ya kuongoza Bunge la Congress kwa kipindi kilichosalia cha urais wa Donald Trump.

Hakuna maoni: