MAKAMU wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi ameshiriki zoezi la upigaji kura katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chamwino huku akihimiza wananchi wa Jimbo la hilo kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia ili kuchagua kiongozi atakayeendeleza maendeleo ya eneo hilo.
Ndejembi ambaye ni mbunge mstaafu wa Jimbo hilo akizungumza baada ya kupiga kura amesema matarajio yake ni kuona idadi ya wapigakura ikiendelea kuongezeka kadiri muda unavyosonga, akibainisha kuwa Chamwino ina historia ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika chaguzi mbalimbali.
Amesema uchaguzi huo ni muhimu kwa wananchi kupata viongozi watakaosimamia ajenda za maendeleo na kuendeleza kazi zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Aidha amesema anaamini wananchi wa Chamwino wana nafasi ya kutathmini maendeleo yaliyotekelezwa katika kipindi cha uongozi wake na kufanya maamuzi kuhusu viongozi wanaotaka waendeleze kazi hiyo.
Amesisitiza kuwa matarajio yake ni kuona wananchi wa vyama vyote wakijitokeza kupiga kura pamoja na tofauti za kisiasa zilizopo lakini wana wajibu wa kujenga Tanzania, Dodoma na Chamwino.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni