Rapper Mabeste na mkewe, Divashia, wamepata mtoto wa kike. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo wa zamani wa label ya B’Hits alichapisha picha akiwa amembeba mwanae na kuandika: “Asante Mungu kwa hii baraka, asante sana mke wangu kwa kunizalia msichana mrembo. #bbygirl I love you so much, Divashia.”
Kwa upande wake, Divashia pia aliweka picha akiwa hospitalini mara baada ya kujifungua huku akiwa amemshika mtoto wao, na kuandika: “Our little angel finally in our arms. #babygirl.”
Mabeste na Divashia, ambao kwa sasa wanaishi nchini Marekani, walifunga ndoa Machi mwaka huu. Kabla ya ndoa yao, Mabeste tayari alikuwa na watoto wawili kutoka ndoa yake ya zamani na Lisa, huku Divashia naye akiwa na watoto wawili wa kike aliowapata katika mahusiano yake ya awali.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni